un’Associazione politico culturale,di cooperazione sociale, sportiva, ricreativa e del tempo libero, senza fini di lucro.
Friday, June 04, 2010
FESTA DEI POPOLI E DELLA SOLIDARIETA' CASTELFRANCO EMILIA
Katibu wa jumuiya ya watanzania Italia Tawi la MODENA ndugu Mwinyimwaka Hatibu pichani akisisitiza umoja baina ya watanzania kupitia chombo maalum cha jumuiya ya watanzania Italia yenye makao makuu mjini NAPOLI. Katibu alisema sherehe kama hizi ni muhimu kwani ni njia mojawapo ya kukutana na kubadilishana mawazo na kuzidisha ushirikiano zaidi. katika kikao hicho cha watanzania kilichofanyika baada ya sherehe za maonyesho pia Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italia Mh.Abdulrahaman A.Alli alipata nafasi ya kusalimiana na watanzania. katika salam hizo mwenyekiti aliwaasa Watanzania kuwa waangalifu na watu wenye nia ya kuharibu umoja wao uliojengeka kwa miaka mingi chini ya uongozi wa jumuiya ya watanzania Italia. pichani katikati ni Mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania Italia tawi la MODENA mh. NYALUSI na pembeni ni ndugu HALIMA MWEVI ambaye ni mweka hazina wa tawi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 MAONI:
Post a Comment